Nov 13, 2020 01:36 UTC
  • Waziri wa  eneo la Jubaland, Somalia anusurika kifo; walinzi wake 2 wauawa

Waziri wa eneo la Jubaland kusini mwa Somalia jana Alkhamisi alinusuruka kifo baada ya mlipuko wa bomu kuyakumbuka makazi yake huko Kismayo kusini mwa mji mkuu, Mogadishu.

Akizungumza na vyombo vya habari, Aidid Suleyman Waziri wa Utalii na Mazingira wa eneo la Jubaland nchini Somalia amethibitisha kutokea mlipuko huo ambao umeuwa watu watatu nyumbani kwake wakiwemo walinzi wake wawili. Aidid Suleyman amesema kuwa amenusurika katika shambulio hilo la bomu. Amesema amesikitishwa na vifo vya walinzi wake wawili na raia mmoja ambao walikuwa nyumbani kwake wakati wa shambulio hilo la kigaidi. 

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulio hilo; hata hivyo wanamgambo wa al Shabaab wenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida  wamekiri kuhusika na mashambulizi mbalimbali ya kigaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Magaidi wa al Shabaab 

Mwezi Julai mwaka huu Waziri wa Masuala ya Kidini na Wakfu wa eneo la Hirshabelle huko Somalia Nur Hashi Warsame aliuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana  katika mji wa Jowhar katika Shabelle ya Kati. Warsame alipigwa risasi baada ya kukamilisha Swala ya Magharibi. Aidha mwezi Machi 2019 Saqar Ibrahim Abdallah Naibu Waziri wa Kazi na Masuala ya Jamii wa Somalia aliuliwa katika shambulio linalofanana na hilo. 

Tags