Nov 23, 2020 13:07 UTC
  • Libya kuanza mazungumzo kwa ajili ya kuyaunganisha mabunge ya mashariki na magharibi mwa nchi

Wabunge wa Libya wanajiandaa kuanza mazungumzo kwa ajili ya kuyaunganisha mabunge mawili ya nchi hiyo yenye makao yao mashariki na magharibi mwa nchi.

Mwakilishi mmoja wa bunge la Libya ameeleza kuwa wabunge wa mabunge hayo yenye makao yao katika miji ya Tobruk na Tripoli  wanajiandaa kushiriki katika kikao maalumu cha kujadili suala hilo.  Mbunge huyo wa Libya ambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la habari la Anadolu kwamba, kikao hicho kimepangwa kufanyika katika mji wa Tangier nchini Morocco; na kitahudhuriwa na wabunge 75 kutoka mabunge yote mawili ya Libya. 

Mbunge huyo aidha amesema, kikao hicho kilikuwa kimepangwa keanza leo Jumatatu. 

Umoja wa Mataifa siku kadhaa zilizopita ulitangaza kuwa, pande zinazozozana huko Libya zilimekubaliana kuendesha chaguzi za bunge na rais Disemba 24 mwaka 2021. Kikao hicho cha Tangier huko Morocco kinafanyika katika hali ambayo mwezi uliopita pande zinazozozana za Libya zilifikia mapatano ya kusimamisha mapigano.

Pande hizo hasimu nchini Libya yaani Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa yenye makao yake katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli na kundi linalojiita Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar, tarehe 23 mwezi Oktoba mwaka huu zilisaini mapatano ya kusimamisha mapigano huko Geneva Uswisi.  

Jenerali muasi, Khalifa Haftar  

 

Tags