Nov 28, 2020 13:44 UTC
  • Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yakataa makundi ya wabeba silaha kuwania viti vya bunge

Mahakama ya Katiba katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza uamuzi wake kuhusu majina ya watu wanaotaka kuwania viti vya bunge katika uchaguzi ujao wa bunge wa Disemba 27 mwaka huu, uchaguzi ambao utafanyika sambamba na ule wa urais.

Mahakama ya Katiba imetoa orodha ya majina ya wagombea 1,585 katika uchaguzi wa bunge, kwa ajili ya kuwania viti 140 katika bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Danielle Darlan, Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, amefutilia mbali majina ya watu kutoka makundi ya wabeba silaha kuwania katika uchaguzi wa bunge.

Kulingana na uamuzi wake, watu zaidi ya hamsini kutoka makundi yenye silaha wamekataliwa kuwania katika uchaguzi wa bunge wa mwezi ujao.

François Bozizé, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika Kati ambaye ametangaza nia ya kkuwania tena kkiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi ujao

 

Wajuzi wa mambo wanasema kuwa, yamkini uAmuzi huo ukachochea mivutano inayoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati juhudi za kieneo na kimataifa zikijaribu kuondokana na hali hiyo baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko kwa miaka kadhaa, wamebaini wadadisi wa mambo.

Machafuko huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yalizuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, François Bozizé. Baada ya Rais Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi wa Kikristo wenye misimamo ya kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu ya Waislamu waliuawa na wengine wengi kulazimika kuwa wakimbizi.