Nov 28, 2020 17:09 UTC

Mahakama ya Katiba katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza uamuzi wake kuhusu majina ya watu wanaotaka kuwania viti vya bunge katika uchaguzi ujao wa bunge wa Disemba 27 mwaka huu, uchaguzi ambao utafanyika sambamba na ule wa urais.

Mahakama ya Katiba imetoa orodha ya majina ya wagombea 1,585 katika uchaguzi wa bunge, kwa ajili ya kuwania viti 140 katika bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Danielle Darlan, Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, amefutilia mbali majina ya watu kutoka makundi ya wabeba silaha kuwania katika uchaguzi wa bunge.

Kulingana na uamuzi wake, watu zaidi ya hamsini kutoka makundi yenye silaha wamekataliwa kuwania katika uchaguzi wa bunge wa mwezi ujao.