Jan 01, 2021 13:25 UTC
  • Walibya wavamia makazi ya kijeshi ya Haftar, wataka kulipiza kisasi dhidi ya mamluki

Wakazi wa mji wa Houn katika eneo la al Jufra huko katikati mwa Libya wamefanya maandamano wakitaka kulipiza kisasi kwa mamluki wa kampuni ya Wagner ya Russia na wapiganaji wa kundi la Janjaweed kutoka Sudan wanaolisaidia jeshi la jenerali muasi, Khalifa Haftar baada ya mauaji ya raia kadhaa wa eneo hilo.

Idara ya Operesheni ya Volkano ya Ghadhabu inayoongozwa na Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imetangaza kuwa, wakazi wa eneo hilo wamefanya maandamano baada ya kukariri vitendo vya uhalifu unaofanywa na mamluki wa Haftar dhidi ya raia. 

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo imesema kuwa, wakazi wa mji huo wamevamia makao ya kijeshi la Jenerali Haftar na kuwataka wapiganaji mamluki kuondoka eneo hilo. Vilevile wametoa wito wa kulipiza kisasi dhidi ya mamluki hao.

Haftar

 

Maandamano hayo yamechochewa na mauaji yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la Janjaweed kutoka Sudan dhidi ya kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Aiman Abu Qasisa.
Wanaharakati wa makundi ya kijamii pia wamesema kuwa raia wengine wawili wameuwa kwa kupigwa risasi au kwa mateso ya mamluki wa Khalifa Haftar na wamewataka raia wa mji huo kuanzisha uasi wa kijamii.

Eneo la al Jufra lina kambi ya jeshi ambayo ripoti zinasema inatumiwa na mamluki wa kundi la Wagner wanaoshirikiana na Khalifa Haftar.    

Tags