Jan 05, 2021 02:18 UTC
  • Vershinin
    Vershinin

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameeleza kuwa waungaji mkono wa dikteta wa zamani wa Libya wanapasa kushirikishwa katika mazungumzo ya amani ya nchi hiyo.

Sergei Vershinin amesisitiza kuwa: Mazungumzo ya amani ya Libya yanapasa kufayika katika fremu ya mazungumzo ya kitaifa kwa kuyashirikisha kadiri inavyowezekana makundi ya kisiasa ya nchi hiyo; wakiwemo waungaji mkono wa Khalifa Haftar, ambaye ni kamanda wa wanamgambo wa kundi linalojiita jeshi la kitaifa la Libya na wafuasi wa Muammar Gaddafi. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kuwa: Mazingira ya mazuri yanapasa kuandaliwa kwa lengo la kufikia mapatano halisi ya kitaifa sambamba na kufanyika uchaguzi wa Libya na kulinda umoja na mshikamano nchini humo. 

Uchaguzi wa Bunge na Rais wa Libya umepangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu. Libya sasa ina serikali mbili; moja ikiwa na makao yake mashariki mwa nchi na nyingine huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo. 

Tags