Jan 18, 2021 08:02 UTC
  • Vikosi vya Ethiopia vyasambazwa katika maeneo ya mipaka ya pamoja na Sudan

Waziri wa Ulinzi wa Sudan ametangaza kuwa wanajeshi wa Ethiopia wamejiweka tayari katika mipaka ya pamoja na Sudan ili kukabiliana na wanajeshi wa nchi hiyo.

Abdulfattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ametangaza katika mkutano na waandishi wa habari huko Khartoum kuwa: Usalama wa bara la Afrika utakabiliwa na tishio iwapo mapigano yatajiri kati ya Sudan na Ethiopia. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan katika jimbo la Darfur Magharibi imeeleza kuwa, watu 83 wameuawa katika mapigano ya kikabila na mashambulizi ya wanamgambo katika mji wa al Janina makao makuu ya mkoa wa Darfur Magharibi, na kuwa idadi ya majeruhi imeongezeka na kufikia 106. 

Kabla ya hapo pia, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia alilituhumu jeshi la Sudan kuwa linatumia vibaya mapigano yanayojiri katika eneo la Tigray kaskazini magharibi mwa Ethiopia kwa lengo la kujipenyeza zaidi katika ardhi ya nchi hiyo. 

Eneo la mpakani baina ya Ethiopia na Sudan hivi karibuni lilikumbwa na mapigano kati ya wanajeshi wa nchi mbili hizo kwa lengo la kulidhibiti eneo la al Fashaga. 

Eeneo la al Fashaga linalogombaniwa na Sudan na Ethiopia 

Nchi mbili za Sudan na Ethiopia zinazozana kuhusu eneo la  ardhi ya kilimo katika eneo la al Fashaga katika mpaka wa kimataifa wa Sudan; eneo ambalo wakulima wa Kiethiopia wanaishi hapo tangu kitambo nyuma. 

Tags