Jan 20, 2021 12:33 UTC
  • Chama tawala Morocco chakabiliwa na wasiwasi wa wimbi la kujiuzulu viongozi wake

Wasiwasi umeongezeka kuhusu wimbi la kujiuzulu viongozi nchini Morocco baada ya kiongozi mtajika ndani ya chama tawala nchini kujiuzulu akilalamimikia hatua ya serikali ya Rabat ya kufikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni.

Abu Zaid al-Muqri al-Idrisi, mmoja wa viongozi mashuhuri wa chama tawala cha  Uadilifu na Ustawi cha Morocco ambacho kinaoongoza muungano tawala nchinu humo tangu mwaka 2012 amejiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho akilalamikia hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kuanzisha uhusiano na Tel Aviv. 

Utawala wa Kizayuni wasaini mapatano na Morocco ya kuanzisha uhusiano 

Abdulaziz Aftati mjumbe wa sekretarieti ya chama tawala cha Uadilifu na Usawa cha Morocco amethibitisha kujiuzulu Abu Zaid al-Muqri al-Idrisi mwanafikira wa Kislamu na mbunge wa chama hicho cha Kiislamu kwa sababu Morocco imeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni.  

Hii ni katika hali ambayo Abu Zaid alikuwa akiungwa mkono pakubwa ndani ya chama hicho tawala cha Morocco cha Uadilifu na Ustawi. 

Tarehe 22 mwezi Disemba mwaka jana Morocco na utawala haramu za Kizayuni wa Israel zilisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano baina yao na kisha Marekani ikatambua rasmi mamlaka ya udhibiti wa Morocco kwa eneo la Sahara Magharibi. 

Umoja wa Mataifa tangu miaka kadhaa nyuma imekuwa  ikiendesha mazungumzo ya kisiasa ili kuainisha mustakbali wa eneo la Sahara Magharibi huko kaskazini mwa Mauritania. Morocco ni nchi ya sita ya Kiarabu baada ya Jordan, Misri, Imarati, Bahrain na Sudan  kuanzisha uhusiano kati yake na utawala ghasibu wa Kizayuni.