Jan 21, 2021 07:41 UTC
  • UN yatoa wito wa kurejeshwa operesheni za uokozi baada ya wahajiri 43 kupoteza maisha

Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya uhamiaji IOM na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yametoa wito kwa nchi kurejesha operesheni za kuwasaka na kuwaokoa watu kwenye bahari ya Mediterania baada ya wahajiri wengine 43 kupoteza maisha katika ajali ya boti iliyotokea siku ya Jumatatu katika pwani ya Libya.

Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jana mashirika hayo mawili yameelezea huzuni yao kwa ajali hiyo mbaya ambayo ni ya kwanza kwa mwaka huu wa 2021 katika Mediterania ya Kati.

Boti hiyo imearifiwa kuzama kutokana na kuchafuka kwa bahari wakati ambapo injini ilizima saa chache tu baada ya kuondoka mjini Zawra Libya Jumanne asubuhi.

Afisa wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM

Manusura 10 ambao wengi wao ni raia wa Ivory Coast, Nigeria, Ghana na Gambia wamearifu kwamba wale waliopoteza maisha wote walikuwa ni wanaume kutoka Afrika Magharibi.

Operesheni za uokozi kwenye bahari ya Mediterania zimepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya karibuni na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yameelezwa kuulaumu Umoja wa Ulaya na nchi wanachama kwa kuongezeka kwa idadi ya vifo katika ukanda huo.../

 

Tags