Jan 22, 2021 08:20 UTC
  • Abiria kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo marufuku kuingia Uingereza

Serikali ya Uingereza imepiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuingia katika nchi hiyo ya bara Ulaya kama moja ya njia za kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

Grant Shapps, Waziri wa Usafirishaji wa Uingereza amenukuliwa akisema kuwa, abiria wote kutoka Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini humo.

Kuanzia tarehe 22 Januari, saa kumi alfajiri wasafiri wote kutoka au wamepita nchini Tanzania ndani ya siku 10 hawataruhusiwi kuingia Uingereza na wale ambao wana haki ya makazi na vibali vya kuishi nchini Uingereza na wanatoka Tanzania watahitaji kukaa karantini na kujitenga nyumbani watakapowasili nchini humo.

Katika masharti mapya nchini Uingereza dhidi ya Corona, lazima watu wabaki nyumbani au kutosafiri, pamoja na kutosafiri nje ya nchi labda tu ukiwa umeruhusiwa kwa kibali maalum kufanya hivyo.

Wakati mataifa mengine yakipambana na janga la Corona Rais wa Tanzania John Magufuli alisema mwezi Juni mwaka jana (2020)kuwa taifa lake 'lipo huru na maambukizi ya virusi vya corona' shukrani kwa maombi.

 

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua ya kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika Kusini.

"Uingereza ilipiga marufuku wasafiri kutoka mataifa 11 ya Afrika Kusini siku 10 zilizopita , mataifa hayo ni pamoja na Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola - visiwa vya ushelisheli na Mauritius," taarifa kutoka idara ya usafirishaji imesema.

Wakati mataifa mengine yakipambana na janga hili Rais wa Tanzania John Magufuli alisema mwezi Juni mwaka jana kuwa taifa lake 'lipo huru na maambukizi ya virusi vya corona' shukrani kwa maombi.