Jan 25, 2021 07:47 UTC
  • Maelfu waachwa bila makao baada ya kimbunga Msumbuji

Kimbunga Eloise kimesababisha maelfu ya watu kuachwa bila makao nchini Msumbuji.

Kwa mujibu wa taarifa kimbunga hicho kilicholeta upepo wa kasi ya kilomita 150 kilisababisha mvua na mafuriko katika mkoa wa Sofala katika pwani ya Msumbuji Jumamosi asubuhi.

Idara ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa nchini Msumbiji imesema watu wapatao 6,859 wameachwa bila makao kufuatia kimbunga hicho hasa katika wilaya ya Buzi. Mashirika ya kutoa misaada yanasema yanahitaji misaada ya dharura ya chakula, maji ya kunywa na makazi ya muda kwa walioathirika. Aidha imekuwa vigumu kuwafikia baadhi ya watu walioathirika katika wilaya ya Buzi kutokana na mafuriko ambayo yamefunga njia zote za mawasiliano.

Hali nchini Msumbujiji baada ya kimbunga

Kimbunge Eloise pia kimeharibu hekari 136,755 za mashamba mbali na kuharibu kabisa shule nane na kusababisha uharibufu usio mkuwa katika shule zingine 17 na hospitali 11. Hali kadhalia nyumba zaidi ya 1000 zimeharibiwa kabisa na kimbunga hicho. Taarifa zinasema kimbunga hicho pia kimesababisha mvua kubwa katika nchi jirani za Zimbabwe, Afrika Kusini na eSwatini.

Mwaka 2019 Msumbuji ilikumbwa na vimbunga viwili Idai na Kenneth ambapo idadi kubwa ya watu wamepoteza maisha na miundomsingi muhimu kuharibiwa huku makumi ya maelfu wakiachwa bila makao.