Feb 15, 2021 01:24 UTC
  • Ethiopia yakubali kwa masharti upatanishi baina yake na Sudan

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa imekubali upatanishi wa nchi nyingine katika mgogoro baina yake na nchi jirani ya Sudan lakini kwa masharti.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Dina Mufti ameitaka serikali ya Sudan kukomesha mashambulizi na kuwafukuza raia wa Ethiopia katika maeneo yao katika operesheni zilizoanza tarehe 6 Novemba wakati Addis Ababa ilipokuwa ikirejesha utawala wa sheria katika eneo la Tigray. 

Dina Mufti amesema kuwa mapigano ya mpakani baina ya Sudan na Ethiopia yaliyoanzishwa na utawala wa Khartoum hayana maslahi kwa taifa la Sudan na wala hayaakisi uhusiano wa siku nyingi baina ya pande hizo mbili. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ethiopia ameashiria mapendekezo ya upatanishi yaliyotolewa na nchi kadhaa ikiwemo Sudan Kusini na kusema: Addis Ababa na Khartoum zinaweza kutatua mzozo huo kwa urafiki baada tu ya jeshi la Sudan kuondoka katika eneo ililolikalia kwa mabavu. 

Jeshi la Sudan

Nchi mbili za Sudan na Ethiopia zinatuhumia kushambulia na kukalia kwa mabavu ardhi ya kila mmoja wao. 

Jumamosi iliyopita Sudan pia iliituhumu Ethiopia kwamba imechukua hatua kama zile za utawala ghasibu wa Israel za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Paletina. Khartoum inasema Ethiopia imevamia na kukalia kwa mabavu eneo la al Fashqa. 

Tags