Feb 28, 2021 08:11 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Kongo

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti na kutahadharisha kuhusu kuendelea mapigano ya silaha na kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu vinavyofanywa na wanamgambo wanaobeba silaha na hivyo kusababisha mamilioni ya watu kuwa wakimbizi.

Umoja wa Mataifa leo umeandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba: Mamilioni ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na kuendelea mapigano na kuongezeka vitendo vya utumiaji mabavu. Tangazo hilo limetolewa baada ya Shirika la Kuhudumia Watoto la UN (Unicef) kueleza kuwa, una wasiwasi kutokana na kuwa hatarini maisha ya watoto wa Kikongo milioni tatu kutokana na kukabiliwa na tishio la wanamgambo wanaobeba silaha nchini humo. 

Wanamgambo wenye silaha wa Kongo 

Gazeti la serikali la La Nation Benin Jumatatu iliyopita liliwanukuu maafisa wa Unicef na kueleza kuwa, wanamgambo wanaoendesha harakati zao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanatishia uhai wa zaidi ya watoto milioni tatu wa nchi hiyo ambao huko nyuma walikuwa wakimbizi kutokana na vita vya ndani. 

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, hivi sasa kuna wakimbizi milioni 5.2 huko Kongo; wengi wao wakitoka katika nchi za Kiafrika. 

Watu 11 wameuawa katika shambulio la karibuni lililotekelezwa katika kambi mbili za jeshi katika mji wa Lubumbashi, mji wa pili muhimu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Wakati huo huo watu zaidi ya milioni 8 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula katika mikoa ya Ituri, Kivu Kusini na Tanganyika ambayo inakabiliwa na hujuma za makundi ya wanamgambo wenye silaha. 

Tags