Mar 05, 2021 08:13 UTC
  • Mogoeng Thomas Mogoeng
    Mogoeng Thomas Mogoeng

Tume ya Mahakama za Afrika Kusini imemwamuru Jaji Mkuu wa nchi hiyo kuomba radhi na kutengua matamshi aliyotoa mwaka jana ambayo yalitambuliwa kuwa yanauunga mkono utawala ghasibu wa Isarel, katika nchi hiyo ya Kiafrika inayotetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina.

Jaji Mkuu wa Afrika Kusini, Mogoeng Thomas Mogoeng alizusha mjadala mkubwa mwezi Juni mwaka jana baada ya kutangaza mapenzi yake kwa Israel na kuuombea dua utawala huo haramu. Jaji Mogoeng alidai kuwa Afrika Kusini inajinyima fursa nzuri ya kuwa mchezaji mkubwa katika kadhia ya Israel na Palestina.

Baada ya matamshi hayo kundi la watetezi wa Palestina liliwasilisha mashtaka rasmi dhidi ya Jaji Mogoeng Thomas Mogoeng kutokana na matamshi yake yanayouunga mkono utawala haramu wa Israel aliyoyatoa katika kongamano la intaneti lililosimamiwa na gazeti la Jerusalem Post likishirikiana na mkuu wa makuhani wa Afrika Kusini, Warren Goldstein.

Tume ya Mahakama ya Afrika ya Kusini iliyofanyia uchunguzi kadhia hiyo imehukumu kwamba matamshi ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo yanadhalilisha na yanazidisha hali mbaya.

Jaji Mogoeng Thomas Mogoeng

Uamuzi wa tume hiyo pia umemtaka Jaji Thomas Mogoeng atengue waziwazi matamshi yake ili kuboresha sura ya mahakama za nchi hiyo.

Afrika Kusini inawaunga mkono watu wa Palestina katika mapambano yao ya ukombozi dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Israel.

Tags