Mar 05, 2021 12:51 UTC
  • Serikali ya Tanzania yatoa indhari juu ya utoaji wa taarifa zinazohusu umma

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbasi amevitaka vyambo habari kuzingatia misingi ya utoaji taarifa.

Katika taarifa yake kwa umma Bw. Abbasi amesema kuwa, katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia ya baadhi ya vyombo vya habari na watu katika mitandao ya kijamii kutoa taarifa bila kuzingatia mwongozo uliowekwa.

''Serikali ina mfumo wake wa kutoa taarifa mbali mbali kwa hiyo wale ambao hawahusiki na taratibu hizo hawafai kuingilia taratibu hizo’’ alisema Bw. Abbas.

Kauli yake inakuja siku kadhaa baada ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania kutangaza  kuwa, limepoteza mapadri 25, watawa na wauguzi 60 kwa matatizo ya kupumua katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Rais Joh Pombe Magufuli, alitangaza Julai mwaka jana (2020) kwamba, Tanzania haina tena virusi vya Corona baada ya siku tatu za maombi ya kitaifa.

 

Tanzania iliacha kutangaza takwimu za maambukizi au vifo vya virusi hivyo mwezi Aprili mwaka jana (2020) baada ya maafisa wa maabara ya taifa kutuhumiwa kutoa matokeo yasiyo sahihi. Aidha Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza Julai mwaka jana kwamba, Tanzania haina tena virusi vya Corona baada ya siku tatu za maombi ya kitaifa.

Aidha ni hivi karibuni tu ambapo, Dakta Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alipoitaka serikali ya Tanzania kutoa taarifa za wagonjwa wa COVID-19 na kutoa takwimu zake.

Dkt. Tedros alisema, baadhi ya Watanzania wanaosafiri kwenda nchi za jirani na kwingineko wamepimwa na kubainika kuwa na virusi vya COVID-19.