Apr 08, 2021 13:03 UTC
  • WHO yasisitiza kuondoa ukosefu wa usawa katika sekta ya afya Afrika baada ya COVID-19

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema, kukabiliana na ukosefu wa usawa ambao unasababisha kuzorota afya kunategemea kuchukuliwa hatua jumuishi na za kasi za baada ya janga la COVID--19 barani Afrika.

Akizungumza katika Siku ya Afya Duniani iliyoadhimishwa jana Jumatano, Moeti amesema janga hilo limevuruga zaidi ukosefu wa usawa katika sekta ya afya barani Afrika, huku watu masikini wakikosa dawa muhimu za kuokoa maisha na kukinga ujauzito.

Amesema kaulimbiu ya Siku ya Afya mwaka huuambayo  ni “Kujenga Dunia ya Usawa na Afya” inasisitiza haja ya kukabiliana na vikwazo vya kifedha na kisera ambavyo vimezuia upatikanaji wa huduma bora za afya barani Afrika.

Mwafrika akipata chanjo ya corona

 

Ameongeza kuwa, unyanyapaa unaotokana na jinsia, kipato, umri, kiwango cha elimu, ukabila na ulemavu vimechochea ukosefu wa usawa wa huduma za afya barani Afrika.