Apr 11, 2021 03:37 UTC
  • Algeria: Ufaransa itaendelea milele kuwa adui wa taifa letu

Waziri wa Kazi wa Algeria ametoa taarifa rasmi na huku akiashiria ripoti zilizofichua kwamba Ufaransa ilifanya majaribio ya nyuklia katika ardhi ya Algeria amesema, mkoloni huyo wa Ulaya ataendelea daima na milele kuwa adui wa taifa letu, kama ambavyo hivi sasa pia Ufaransa ni adui mkongwe na wa zamani sana wa Algeria.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu el Hachemi Djaaboub akisema hayo na kuongeza kuwa, jeshi la Algeria limeitaka Ufaransa iwalipe fidia wananchi wa Algeria kutokana na kufanya majaribio ya nyuklia katika ardhi ya nchi hiyo miaka 60 iliyopita na kuhatarisha usalama wa wananchi wa Algeria tangu wakati huo hadi hivi sasa.

Hivi karibuni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alifanya ujanja wa kisiasa wa kuvutia kura za milioni kadhaa za wananchi wa Ufaransa wenye asili ya Algeria kwa kudai kuwa Parisa ilifanya kosa kufanya majaribio ya nyuklia katika ardhi ya Algeria miaka 60 iliyopita. Alisambaza pia nyaraka za kihistoria zinazothibitisha jinai hiyo ya dola vamizi na la kikoloni la Ufaransa dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Algeria.

Maafa ya jinai ya nyuklia ya Ufaransa yanawatesa hadi leo wananchi maskini wa Algeria

 

Naam, karibu miaka 60 iliyopita, Ufaransa ilifanya majaribio ya nyuklia katika baadhi ya maeneo ya Algeria. Majaribio hayo yaliyaweka maisha ya wanavijiji na wakazi wa maeneo hayo katika hatari kubwa. Wananchi hao maskini wa Algeria walifanyiwa majaribo hayo ya nyuklia na mkoloni kizee Ufaransa ili mkoloni huyo mtenda jinai aweze kujua athari za mionzi ya nyuklia kwa wakazi wa maeneo yanapofanyika majaribio ya atomiki.

Tags