Apr 15, 2021 02:55 UTC
  • Mkuu wa Baraza la Urais Libya apinga kufikiwa makubaliano yoyote

Mkuu wa Baraza la Urais la Libya amesisitiza kuwa baraza hilo haliwezi kufikia makubaliano yoyote kwa mujibu wa mapatano ya pamoja yaliyofkiwa katika mazungumzo ya kisiasa ya nchi hiyo huko Geneva Uswisi.

Mohamed Yunus al-Menfi Mkuu wa Baraza la Urais la Libya amesisitiza umuhimu wa kuhuisha na kuanzisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika nyanja za kiuchumi na kiutamaduni na kuyaalika mashirika mbalimbali ili kushirikiana katika sekta ya umeme na nishati jadidifu. Mohamed al Menfi ameyasema hayo jana katika mazungumzo na Rais Katerina Sakellaropoulou wa Ugiriki. 

Al Menfi katika mazungumzo na Rais wa Ugiriki 

Al Menfi ameongeza kuwa, anafanya juhudi zote ili kuhakikisha kuwa Libya inajitawala na kuwa huru kwa kuondoka kikamilifu wanamgambo wa nchi za nje nchini humo. 

Mkuu wa Baraza la Urais la Libya alielekea Ugiriki katika ziara yake rasmi nchini humo kwa lengo la kuchunguza masuala ya pande mbili na masuala muhimu zaidi ikiwa ni makubaliano kuhusu masuala ya bahari yaliyosainiwa na nchi mbili za Uturuki na Libya; ambayo yanalalamikiwa na Ugiriki.