Apr 17, 2021 07:35 UTC
  • Wanigeria wataka kuachiwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky

Mamia ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria (IMN), wamefanya maandamano wakitaka kuachiwa huru kiongozi wa harakati hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, Mallimah Zeenah.

Ofisi ya Sheikkh Zakzaky imetangaza kuwa, wafuasi wa kiongozi huyo walifanya maandamano makubwa jana katika mji mkuu wa Nigeria wakitaka kuachiwa huru kiongozi huyo na mke wake bila ya masharti yoyote. 

Maandamano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila wiki yamefanyika katika kitongoji cha Garki mjini Abuja. 

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake walitiwa nguvuni tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya kituo cha kidini cha Baqiyyatullah katika mji wa Zaria.

Mauaji ya Waislamu katika mji wa Zaria

Mamia ya Waislamu waliuawa shahidi katika shambulizi hilo wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky.

Serikali ya Nigeria inadai kuwa, kiongozi huyo wa Kiislamu na mkewe wanakabiliwa na tuhuma za mauaji, kuitisha maandamao haramu na kuvuruga usalama. 

Hata hivyo tarehe 2 Disemba 2016 Mahakama Kuu ya Nigeria ilitoa hukumu kwamba, kutiwa mbaroni Sheikh Zakzaky na mkewe ni kinyume cha sheria na kunakinzana na katiba ya nchi hiyo, hivyo wanapaswa kuachiwa huru. Serikali ya Abuja imekataa kutekeleza hukumu hiyo. 

Tags