Apr 22, 2021 04:31 UTC
  • Wapinzani nchini Chad wapinga mtoto wa Idris Deby kuongoza nchi

Vyama vikuu vya upinzani nchini Chad vimepinga uteuzi wa mtoto wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Idris Deby ,Mahamat Deby kuwa kiongozi wa taifa hilo wakisema kwamba, hayo ni "mapinduzi ya kitaasisi".

Mbali na vyama vya upinzani, waasi pia wamepinga hatua hiyo, wakisema kuwa "Chad sio nchi ya ufalme." Serikali na bunge vimevunjwa, lakini wataalamu wa katiba wanasema kuwa, kwa mujibu wa katiiba Spika wa bunge ndiye anayepaswa kuchukua nafasi ya uongozi wa nchi  kabla ya kuitishwa uchaguzi wakati rais aliye madarakani anapofariki au anaposhindwa kuongoza nchi.

Aidha muungano wa vyama vya wafanyakazi umejiunga na upinzani kukataa kuanzishwa kwa Baraza la mpito la jeshi, wakitaka mazungumzo, na wafanyakazi wakae nyumbani hadi hapo mwafaka utakapopatikana 

Idriss Deby aliaga dunia juzi  kutokana na majeraha aliyoyapata katika medani ya vita.

Idris Deby aliyekuuwa Rais wa Chad 

 

Deby aliuawa akipambana na magaidi waliotokea nchi jirani ya Libya huko kaskazini mwa Chad alikokwenda kukagua jeshi la nchi hiyo linalopigana na makundi ya kigaidi.

Idriss Deby ambaye ameiongoza Chad kwa kipindi cha miaka 30, ameuawa kabla ya kuapishwa kuingoza nchi hiyo kwa awamu ya sita baada ya Kamisheni ya Uchaguzi kumtangaza mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 11 mwezi huu wa Aprili.

Wapinzani watoa malalamiko mhayo katika hali ambayo nchini Chad tayari kumeundwa Baraza la Kijeshi linaloongozwa na mtoto wa kiume wa Rais Idriss Deby, Jenerali Muhammad Idriss Déby Itno (maarufu kama Mahamat Kaka) litakaloongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito cha miezi 18.