Apr 22, 2021 11:22 UTC
  • Kimbunga Jobo kinaelekea Tanzania, ni cha aina yake tokea 1952

Kimbunga kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Tanzania miongo ya karibuni kinatazamiwa kutua katika ukanda wa pwani ukiwemo mji wa Dar es Salaam na Zanzibar.

Kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya utabiri wa hali ya hewa, kimbunga hicho ambacho kinajulikana kama Jobo kinatarajiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutua Tanzania tangu mwaka 1952.

Kwa mujibu wa taarifa, jana kimbunga hicho kilionekana kaskazini mwa Madagascar kikiwa na kasi ya kilomita 83 kwa saa.

Utabiri unaonyesha kuwa kimbunga hicho kitapita eneo la Ushelisheli leo Aprili 22 kikiwa na kasi ya kilomita 130 kwa saa na kinatazamiwa kutua Tanzania Aprili 24 au 25.

Upepo mkali wakati wa kimbunga

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMAimetahadahrisha kuwa kimbunge hicho cha Bahari ya Hindi kinaweza kusababisha upepo mkali na mawimbi makubwa baharini katika maeneo ya Lindi na Mtwara. Aidha kuna uwezekano wa kutokea mafuriko katika maeneo athirika.

TMA imesema itaendelea kufuatilia kimbunga Jobo na kuwapasha wananchi habari kuhusu tahadhari zinazopasa kuchukuliwa.