May 10, 2021 12:35 UTC
  • Algeria yalitaka Baraza la Usalama la UN kuwahami Wapalestina katika Msikiti wa al Aqsa

Wizara ya Mambo Nchi za Nje ya Algeria imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liwahami na kuwalinda Wapalestina wanaofanya itikafu ndani ya Msikiti wa al Aqsa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Algeria imeashiria hujuma ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na imelitaka Baraza la Usalama la UN kuchukua hatua za haraka za kuwahami Wapalestina na maeneo yao matukufu.

Algeria pia imetangaza mshikamano na himaya yake kwa taifa la Palestina katika mapambano yake dhidi ya wavamizi na askari madhalimu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa siku kadhaa sasa askari wa Israel wamekuwa wakishambulia Msikiti wa al Aqsa na viunga vyake ambako makumi ya raia wa Wapalestina wanaendelea kufanya ibada na itikafu kwa mnasaba wa kuhuisha usiku wa Lailatul Qadr.  

Askari wa Israel wakishambulia Msikiti wa al Aqsa

Hujuma na mashambulizi ya askari wa Israel huko Quds yameshadidi zaidi tangu Ijumaa iliyopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Palestina ilmetangaza kuwa, Wapalestina wasiopungua 208 wamejeruhiwa katika hujuma na mashambulizi ya wanajeshi wa Israel dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na viunga vyake.    

Tags