Jun 03, 2021 08:11 UTC
  • Algeria yapinga tena kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni

Rais wa Algeria jana usiku kwa mara nyingine amesisitiza kuwa, nchi yake abadan haitaanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.

Rais Abdelmajid Tebboune amepinga hatua yoyote ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, Algiers inaunga mkono malengo ya wananchi wa Palestina.

Algeria, tofauti na nchi jirani ya Morocco, imepinga kuanzisha kivyovyote vile uhusiano na utawala ghasibu wa Israel. Algeria imekuwa ikisisitiza msimamo wake imara na madhuuti wa kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.  

Abdelmajid Tebboune ametahadharisha pia kuhusu harakati zinazoibuka tena za magaidi huko Mali na kueleza kuwa  Algeria kamwe haitaruhusu eneo la Kaskazini mwa Mali kutumiwa kama maficho ya magaidi.  

Sudan, Imarati na Bahrain pia zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel. Hatua hiyo imepingwa na kukosolewa pakubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu. 

Itakumbukwa kuwa, nchi nne yaani Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco  mwaka 2020 zilifikia mapatano rasmi na utawala ghasibu wa Israel ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kufuatia mashinikizo ya Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump.  

Wawakilishi wa Bahrain na Imarati wakisaini mapatano na Israel huko Washington

 

Tags