Jun 13, 2021 07:33 UTC
  • Rais wa Nigeria akiri kushindwa kukabiliana na Boko Haram

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amekiri kushindwa kuwamaliza magaidi wa Boko Haram na kuwaletea amani wananchi wa nchi hiyo.

Shirika la habari la Reuters limemnukuu Buhari akisema hayo katika mahojiano ya televisheni na kuongeza kuwa, vita dhidi ya wanamgambo wa kaskazini mwa nchi vimeleta matokeo yasiyofurahisha. Vimechochea machafuko katika maeneo mengine ya Nigeria.

Baada ya kuchaguliwa kura rais wa Nigeria mwaka 2015, Buhari alisema kuwa, jeshi la Nigeria limefanikiwa kulishinda kiufundi genge la magaidi wa Boko Haram.

Hata hivyo mwaka huo huo genge hilo lilizidisha mashamblio yake mashariki mwa Nigeria kwa kushambulia kambi kadhaa za kijeshi likateka maeneo kadhaa na kuiba silaha, vyakula na madawa.

Magaidi wa Boko Haram wanafanya jinai nyingi nchini Nigeria

 

Genge la kigaidi la Boko Haram lilipanua mashambulizi yake pia hadi katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Niger mwaka huo huo wa 2015. Cha kusikitisha ni kuwa wahalifu wengine nao wanatumia vibaya hali hiyo kuteka watu nyara, kuiba, kufanya uharibifu wa mali za watu, kulipiziana kisasi na maovu mengine mengi.

Cha kusangaza ni kuwa, badala ya kuelekeza nguvu zake kuleta amani na kupambana na magaidi wa Boko Haram, serikali ya Muhammadu Buhari inawasakama Waislamu wasio na madhara kwa taifa kama inavyowakandamiza wanachama wa Jumuiya ya Kiislamu ya nchi hiyo na kuendelea kumshikilia gerezani kinyume cha sheria, kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky aliyekamatwa na jeshi la Nigeria baada ya kupigwa risasi kadhaa na kusababishiwa madhara makubwa mpaka kwenye macho yake.