Jun 16, 2021 02:35 UTC
  • Kero la ugaidi; 50 wauawa Burkina Faso na Nigeria

Jeshi la Burkina Faso limetangaza kuwa magaidi 25 wameuliwa katika operesheni iliyofanywa na askari wa jeshi hilo.

Taarifa ya jeshi la Burkina Faso imeeleza kwamba, magaidi hao waliuawa katika operesheni iliyofanyika baina ya Juni 7 na 13.

Duru za jeshi la Bukina Faso zinasema kuwa, wanajeshi watatu wa serikali na sita wa kujitolea wameuawa pia katika operesheni hiyo dhidi ya magaidi.

Haya yanajiri siku chache baada ya watu zaidi ya 130 kuuawa katika hujuma ya wabeba silaha katika kijiji cha Solhan mkoani Yagha, mpakani mwa nchi hiyo na Niger, usiku wa kuamkia Juni 6.

Katika hatua nyingine, watu wasiopungua 25 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi mawili toafuti yanayosadikika kuwa ya kigaidi huko nchini Nigeria.

Magenge ya wabeba silaha yanayowahangaisha wananchi wa Nigeria

Kwa akali watu 11 wamepoteza maisha kwenye shambulizi la kwanza la wabeba silaha katika mkoa wa Agatu ulioko jimbo la Benue, kaskazini mwa nchi.

Kadhalika watu 14 wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana katika mkoa wa Bassa ulioko jimbo la Plateau, katikati mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Tags