Jun 17, 2021 06:51 UTC
  • UN yakosoa mienendo ya vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewakosoa vikali maafisa usalama wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa kile alichokitaja kuwa kushtadi mienendo ya kiuhasama na vitisho dhidi ya askari wa kulinda amani wa umoja huo nchini humo.

Katika ripoti mpya ya kurasa 37 kwa Baraza la Usalama la UN, Antonio Guterres amesema wananchi wa CAR wangalia wanakabiliwa na wimbi kubwa na lisilokubalika la ghasia na mapigano.

Guterres ameashiria ukiukwaji wa haki za binadamu, na kumtaka Rais wa nchi hiyo, Faustin Archange Touadera kutumia muhula wake huu wa pili wa uongozi kutafuta kiini cha migogoro nchini humo.

Kadhalika Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka rais huyo ambaye mapema mwaka huu, Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo, iliidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Disemba 27 mwaka jana, atoe kipaumbele kwa amani na maridhiano.

Mgogoro wa wakimbizi uliosababishwa na ghasia CAR

Jamhuri ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa madini imekuwa katika mgogoro na mapigano ya kidini na kikabila tokea mwaka 2013.

Baada ya Rais Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi wa Kikristo wenye misimamo ya kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu.

Tags