Jul 19, 2021 13:32 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa China: Kuasisiwa nchi huru ya Palestina ni haki ya kisheria ya Wapalestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema kuwa, kuundwa nchi huru ya Palestina ni haki ya kisheria ya Wapalestina na jambo hilo halipasi kuakhirishwa.

Akizungumza mjini Cairo na Sami Shoukry Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri pamoja na Ahmad Abul Ghait Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), Wang Yi Waziri wa Mambo ya Nje wa China ameeleza kuwa, kuundwa nchi huru ya Palestina hakupasi kuwa jambo la kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu kadhia hiyo ni haki ya kisheria ya watu wa Palestina na haipasi kupuuzwa kwa muda mrefu. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ametilia mkazo suala la kurejeshwa amani huko Palestina. 

Kwa upande wao Shoukry na Abul Ghait wameashiria nafasi ya China katika kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina na wameunga mkono matamshi ya Wang Yi kuhusu Palestina. Pande mbili hizo zimesema zipo tayari kutoa ushirikiano katika uwanja huo. 

Siasa za kuangamiza kizazi zinazotekelezwa na Israel ikikingiwa kifua na kusaidiwa kwa hali na mali na Marekani zimezimezidisha masaibu na mashaka kwa wananchi wa Palestina tangu miaka 74 nyuma. 

Utawala wa Kizayuni wa Israel pia tarehe 10 Mei mwaka huu ulianzisha vita vipya dhidi ya Wapalestina huko Quds, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza. Tarehe 21 mwezi huo wa Mei baraza la mawaziri wa Israel liliomba kusimamishwa vita hivyo baada ya kupata kipigo kutoka ka wanamapambano wa Kipalestina. 

Vita vya siku 12 vya Israel dhidi ya Ghaza 

 

Tags