Jul 25, 2021 11:23 UTC
  • Wapiganaji wa eneo la Tigray Ethiopia watishia kuelekea Addis Ababa

Harakati ya Ukombozi ya eneo la Tigray (TPLF) imesema wapiganaji wa harakati hiyo ya kaskazini mwa Ethiopia hivi sasa wapo katika hali na nafasi nzuri ya kusonga mbele na kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa.

Jenerali Tsadkan Gebretensae, afisa wa ngazi ya juu wa TPLF amesema wapiganaji wa harakati hiyo wamekamilisha operesheni ya siku tatu katika eneo la Kobbo-Weldiya jimbo la Amhara, na eti wamefanikiwa kudhibiti miji miwili ya eneo hilo.

Ameongeza kuwa, wamefanikiwa kuangamiza kikosi cha Gadi ya Rais kilichotumwa kukabilana nao na kwamba baada ya mafanikio hayo, hivi sasa mlingano wa nguvu upo kwa maslahi yao na wanaweza kuelekea Addis Ababa. 

Kamanda huyo wa wapiganaji wa TPLF amesema wameptaka mafanikio makubwa katika makabliano yao katika barabara ya mji wa Chercher kuelekea Mille eneo la Afar, na sasa hawana kipingi cha kelekea katika mji mkuu wa nchi.

Kifaru cha kijeshi katika eneo la Tigray

Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya watu 20 kuuawa katika mapigano ya silaha yaliyojiri karibu na eneo hilo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia.

Aidha watu wengine elfu 70 wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na mapigano hayo kati ya waasi na wapiganaji wanaoiunga mkono serikali kuu ya Addis Ababa, katika eneo la Afar karibu na Tigray kaskazini mwa Ethiopia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kutekelezwa usitishaji vita katika eneo la Tigray na kuwezesha misaada ya kibinadamu kupelekwa katika eneo hilo. 

Tags