Jul 26, 2021 02:39 UTC
  • Wanaharakati wa nchi 5 za kaskazini mwa Afrika: Kuna udharura wa kukabiliana na mwenendo wa kuanzisha uhusiano na Israel

Wanaharakati kutoka nchi tano za kaskazini mwa Afrika ambazo ni Algeria, Tunisia, Morocco, Libya na Mauritania wamesisitiza udharura wa kukabiliana na hatua ya baadhi ya nchi ya kuanzisha uhusiano rasmi wa na utawala ghasibu wa Israel.

Wanaharakati na taasisi mbalimbali huko Algeria, Tunisia, Morocco, Libya na Mauritania wamesema wanapinga suala la kuanzishwa uhusiano kati ya nchi hizo na utawala wa Kizayuni na wametoa wito wa kuwepo mshikamano baina watu wa nchi hizo na kuwa na mkakati wa pamoja kwa ajili ya kukabiliana na hatua hiyo ambayo ni tishio kwa usalama wa nchi zenye mpaka na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, nchi za Kiislamu na  Kiarabu. 

Muhammad al Ghafuri mratibu wa Mtandao wa Kidemokrasia kwa Ajili ya Mshikamano na Mataifa Mbalimbali wenye makazi yake huko Morocco amesema kuwa, mataifa ya Kiarabu yanapinga suala la kuanzishwa uhusiano kati ya tawala za Kiarabu na Israel licha ya baadhi ya nchi za Kiarabu kufanya hiyo. Amesema kuwa mataifa ya Kiarabu yako pamoja na wananchi wa Palestina. 

Al Ghafuri ameongeza kuwa, ni jambo la kuhuzunisha kuona Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) unafungua ubalozi huko Israel.

Katika upande mwingine, Ahmad Ibrahimi mratibu wa Harakati ya Wananchi Inayopinga Kuanzisha Uhusiano na Utawala wa Kizayuni huko Algeria ameeleza kuwa, kuanzisha uhusiano na utawala huo ni jinai na uhalifu dhidi ya wananchi wa Palestina na usalama wa Waarabu na Waislamu. Amesema ni jukumu la nchi za Kiarabu na Kiislamu kupambana na hatua hiyo.  

Miezi kadhaa iliyopita Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco zilianzisha waziwazi uhusiano na utawala wa Kizayuni; hatua iliyopingwa na kukosolewa vikali na makundi ya mapambano ya Palestina na nchi mbalimbali duniani. 

Imarati na Bahraini zikisaini hati ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni huko Washington 

 

Tags