Jul 26, 2021 03:08 UTC
  • Rais wa Tunisia afanya mapinduzi baridi, amfuta kazi Waziri Mkuu, Spika wa Bunge

Rais Kais Saied wa Tunisia amechukua hatua ya kushtukiza ya kumfuta kazi Spika wa Bunge na Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kudhibiti madaraka yote ya nchi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Tunisia imesema kuwa, Rais Kais Saied amechukua uamuzi wa kuongoza baraza la mawazri yeye mwenyewe, na sambamba na kusitisha shughuli za Bunge, vilevile amefuta kinga ya kisiasa ya wabunge wote.

Baadhi ya duru zinasema kuwa, Rais huyo wa Tunisia amefanya mapinduzi baridi akishirikiana na jeshi la nchi hiyo. 

Spika wa Bunge la Tusia, Rached Ghannouchi ameitaja hatua ya rais wa nchi hiyo kuwa ni mapinduzi dhidi ya mapinduzi ya wananchi, katiba ya nchi na uhuru wa taifa.

Kwa sasa Tunisia inakabiliwa na mandamano makubwa ya wananchi wanaopinga kufutwa kazi aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Hichem Mechichi. 

Mapinduzi baridi ya Rais Kais Saied nchini Tunisia yamefanyika huku mamia ya watu wakifanya maandamano jana Jumapili kulalamikia hali mbaya ya kisiasa na ukosefu wa huduma za afya. 

Mapema jana njia zote zinazoishia mji mkuu wa Tunisia, Tunis, zilifungwa, na idadi kubwa ya wanajeshi ilionekana katika barabara kuu za nchi hiyo. 

Tags