Jul 27, 2021 03:19 UTC
  • Polisi yaivamia ofisi ya Al Jazeera huko Tunis

Mkuu wa ofisi ya televisheni ya al Jazeerahuko Tunis mji mkuu wa Tunisia amesema polisi wameivamia ofisi hiyo jana Jumatatu.

Amesema, polisi 20 jana walivamia katika ofisi hiyo ya al Jazeera na kuwafukuza wana habari na maripota wa televisheni hiyo na kisha kusitisha shughuli zake. Hii ni katika hali ambayo wafanyakazi wa ofisi ya televisheni ya al Jazeera huko Tunis walikuwa hawajapewa taarifa wala tahadhari yoyote mapema kuhusu kujiri tukio hilo. Shambulio hilo limejiri baada ya juzi jioni Rais wa Tunisia Kais Saied kumfuta kazi Waziri Mkuu Hichem Mechichi; hatua iliyotajwa na wapinzani kuwa ni mapinduzi baridi. 

Polisi ya Tunisia imevamia ofisi ya televisheni ya al Jazeerahuko Tunisia bila ya kibali.   

Askari polisi wa Tunisia waliohusika katika uvamizi huo wamesema kuwa wametekeleza maagizo waliyopewa na vyombo vya mahakama vya nchi hiyo.maripota wa al Jazeera wameeleza kuwa, maafisa usalama wa Tunisia waliwaamuru kuzima simu zao na hawakuruhusiwa kurejea katika jengo la ofisi yao kuchukua suhula zao. 

Makabiliao ya polisi na maripota wa al Jazeera 

Kwa upande wake televisheni ya al Jazeera imelitaja shambulio hilo dhidi yake kuwa ni shambulio dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

 

Tags