Jul 27, 2021 07:34 UTC
  • Wahajiri 57 waaga dunia katika pwani ya Libya

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limetangaza kuaga dunia wahajiri 57 katika pwani ya Libya baada ya kupinduka na kuzama boti waliyokuwa wakisafiria.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limetangaza kuwa, wahajiri wasiopungua 57 wameaga dunia katika pwani ya Libya baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama. Wanawake na watoto karibu 20 ni kati ya wahajiri walionusika na ajali hiyo ya kuzama boti ambao waliokolewa kwa msaada wa boti za wavuvi na walinzi wa pwani ya Libya. 

Walinzi wa pwani ya Libya

Shirika la Kimataifa la Wahajiri ni kati ya mashirika yaliyo chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Aghalabu ya wahajiri kutoka katika nchi za Kiafrika na za eneo la Magharibi mwa Asia katika miaka ya karibuni wameaga dunia kufuatia kuzama boti zao katika maji ya Mediterania wakiwa katika juhudi za kuelekea barani Ulaya. Wahajiri hao huku wakiwa katika boti za wanaojihusisha na magendo ya binadamu hujaribu kuelekea Ulaya wakitaraji kuwa  wakifika huko watakuwa na maisha bora kutokana na matatizo mbalimbali ya kiusalama na kiuchumi yanayozikabili nchi walikotoka. Wahajiri hao huhatarisha maisha yao kwa kufanya safari hizo katika bahari ya Atlantic au Mediterania kuelekea katika nchi za Ulaya. 

Tags