Jul 29, 2021 10:28 UTC
  • Uchunguzi: Wanasiasa waliojitokeza kuwania kiti cha rais 2022 hawana jipya kwa Wakenya

Tathmini ya rekodi za kisiasa iliyofanyika huko Kenya inaonyesha kuwa wanasiasa wakuu wanne waliotangaza nia ya kuwania urais mwaka ujao hawana kipya cha kuwafaa Wakenya.

Naibu Rais William Ruto, Kiongozi wa ODM Raila Odinga, Musalia Mudavadi  wa chama cha ANC na Kalonzo Musyoka  wa chama cha Wiper wamejitokeza kama wawaniaji wakuu katika uchaguzi ujao kwa ahadi za kuboresha maisha ya Wakenya wa kawaida hasa kiuchumi iwapo watachaguliwa 2022.

Hata hivyo rekodi za wanasiasa hao katika ulingo wa siasa zinaonyesha kuwa, hujali maslahi ya mwananchi wakati wa msimu wa uchaguzi, na mara wanapochaguliwa wanazingatia maslahi yao ya kibinafsi na ya washirika na jamaa.

Mdadisi wa siasa nchini Kenya, Javas Bigambo anasema: “Kwa vigogo hao, siasa ni kama biashara. Ni jukwaa ambalo wamekuwa wakilitumia kujitajirisha, kulinda na kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi. Ahadi ambazo huwa wanatoa nyakati za uchaguzi kuhusu mikakati ya kumsadia mwananchi ni njama za kuwapumbaza wapiga kura”.

Wawaniaji wa kiti cha rais Kenya

Taarifa zinaonesha kuwa, vigogo hao wanne wamekuwa katika bunge na serikali mbalimbali kwa miaka mingi na wameshikilia vyeo vya juu vilivyowapa nafasi za kutekeleza ajenda za kumsaidia mwananchi, lakini hawakufanya hivyo.

Vigogo hao wote pia waliwahi kuwa makamu wa rais isipokuwa Bw. Odinga, ambaye naye alishikilia cheo kikubwa zaidi cha waziri mkuu.

Wadasisi wa siasa nchini Kenya wanawashauri wananchi kuwachagua viongozi kwa kuangazia sifa za utendakazi wao. Uchaguzi mkuu wa Kenya umepangwa kufanyika mwaka 2022. 

Tags