Jul 30, 2021 12:43 UTC
  • Namibia pia yalaani kuruhusiwa Israel kuwa mwanachama wa AU

Namibia imelalamikia vikali kitendo cha kuruhusiwa utawala haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika (AU).

Katika taarifa leo Ijumaa, Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia imesema serikali ya nchi hiyo ya Kiafrika imehamakishwa na kutiwa wasi wasi kutokana na hatua ya kutambuliwa utawala haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika.

Taarifa hiyo, kwa mujibu wa shirika la habari la Anadolu la Russia imeeleza bayana kuwa, kuruhusiwa Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa AU kumeenda sambamba na utawala wa Kizayuni kushadidisha mashinikizo na mbinyo dhidi ya wananchi wa Palestina.

Imesisitiza kuwa, uamuzi huo wa kuudhinisha utawala haramu kuwa mwanachama wa mtazamaji wa AU unakinzana moja kwa moja na malengo na thamani za umoja huo wa kibara.

Maandamano ya kutaka kususiwa Israel

Aidha taarifa ya Wizara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya Namibia imeashiria kuhusu uungaji mkono wa nchi hiyo ya Kiafrika kwa wananchi madhulumu wa Palestina mkabala wa utawala ghasibu wa Israel. 

Hivi karibuni, Afrika Kusini na Algeria zilitangaza pia kupinga kitendo cha kutambuliwa utawala haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika. Julai 22, utawala haramu wa Israel ulitangaza kuwa umeidhinishwa kuwa mwanachama mtazamaji wa AU baada ya eti jitihada za kidiplomasia za karibu miongo miwili.

Tags