Jul 31, 2021 07:37 UTC
  • Wamorocco wapinga safari za watalii wa Israel nchini kwao

Maelfu ya wananchi wa Morocco wameanzisha kampeni kubwa ya kupinga safari za wataali wa Israel katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Kampeni hiyo inayofanyika kwa anwani ya "Wazayuni hawakaribishwi nchini Morocco' inawashirikisha maelfu ya wananchi wa Morocco katika mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Ripoti zinasema kuwa, kampeni hiyo imeanzishwa baada ya shirika la ndege la Yasrair kutangaza kwamba, limeanzisha safari za ndege baina ya Israel na Morocco na kwamba safari hiyo ilikuwa ya kwanza baada ya pande hizo mbili kufanya makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia.

Msemaji wa shirika la ndege la Yasrair, Tali Leibovich amesema kuwa, safari hiyo ya kwanza ilikuwa na wasafiri mia moja. 

Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Yair Lapid ametanga nia yake ya kuitembelea Morocco mwanzoni mwa mwezi ujao wa Agosti baada ya kuzinduliwa safari ya kwanza ya ndege baina ya pande hizo mbili. 

Morocco ni nchi ya sita ya Kiarabu baada ya Jordan, Misri, Imarati, Bahrain na Sudan  kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Kizayuni. 

Kitendo hicho cha Morocco cha kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel ambacho ni sawa na kusaliti malengo ya Palestina kimekabiliwa na upinzani mkubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu na hata ndani ya Morocco kwenyewe. 

Tags