Jul 31, 2021 13:56 UTC
  • Barua ya HAMAS kwa Umoja wa Afrika kulalamikia Israel kupasishwa kuwa mwanachama mtazamaji wa AU

Mkuu w Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amemuandikia barua Mossa Faki, Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika akilalamia hatua ya umoja huo ya kuuteua utawaa haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa umoja huo.

Katika barua yake hiyo, Ismail Hania sambamba na kupongeza misimamo ya kihistoria ya Umoja wa Afrika katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina ameshangazwa mno na uamuzi wa umoja huo wa kuuteua utawaa haramu wa Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa Umoja wa Afrika.

Sehemu nyingine ya barua ya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS kwa Moussa Faki inasema, Umoja wa Afrika wenye historia kongwe daima umekuwa ukiunga mkono haki za Waafrika za kujiaianisha mambo yao na kuwa na uhuru na mamlaka ya kujitawala na  umekuwa pamoja na wananchi wa Palestina dhidi ya uvamizi na ugaidi, lakini uamuzi wa hivi karibu wa kuifanya Israel mwanachama mtazamaji wa jumuiya hiyo unakinzana wazi na thamani na misingi ya Umoja wa Afrika.

Nembo ya Umoja wa Afrika

 

Ismail Hania amesisitiza kuwa, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na wananchi wa Palestina kwa ujumla wanalalamikia na kulaani vikali uamuzi huo wa Umoja wa Afrika.

Hatua ya Umoja wa Afrika ya kuiteua Israel kuwa mwanachama mtazamaji wa umoja huo wenye makao yake makuu mjini Addis Ababa Ethiopia imeendelea kulalamikiwa hata na nchi wanachama wa jumuiya hiyo kubwa zaidi barani Afrika ambapo Algeria na Namibia zimejitokeza na kulalamikia vikali uamuzi huo.