Aug 01, 2021 03:00 UTC
  • Kesi za Corona barani Afrika zapindukia milioni 6 na laki 6

Idadi ya kesi za ugonjwa wa Covid-19 (Corona) zilizothibitishwa katika nchi za Afrika kufikia jana Jumamosi imepindukia laki sita.

Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) ambazo zinaonyesha kuwa, kesi 6,678,949 za ugonjwa wa Covid-19 zimenakiliwa barani Afrika kufikia jana Jumamosi, huku idadi ya vifo ikifikia 169,280.

Kituo hicho kimesema licha ya virusi vya Corona aina ya Delta kuenea kwa kasi katika nchi za Afrika kama vile katika nchi nyingine duniani, lakini habari njema ni kwamba wagonjwa zaidi ya 5,845,926  wa Corona wamepata afueni barani humo.

Kwa mujibu wa Africa CDC, nchi zilizoathiriwa zaidi na janga la Corona ni zile za kaskazini mwa bara hilo za Misri, Tunisia, Morocco, Algeria pamoja na Afrika Kusini na Ethiopia.

Tahadhari kabla ya hatari katika shule za Afrika

 

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ni asilimia moja tu ya watu wa bara la Afrika ndio waliopata chanjo kamili ya Covid-19 hadi kufikia sasa, huku nchi za bara hilo zikiendelea kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chanjo hizo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa asllimia 90 ya malengo ya chanjo ya kutoa chanjo ya virusi vya Corona barani Afrika bado haijatekelezwa.

Tags