Aug 04, 2021 07:02 UTC
  • Watu 37 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Mali

Serikali ya Mali imetangaza kuwa watu 37 wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea katikati mwa nchi hiyo.

Taarifa ya serikali ya Bamako imeeleza bila kutoa ufafanuzi zaidi kwamba, watu 37 wamefariki na wengine wengi wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea katikati mwa nchi hiyo.

Baadhi ya duru nchini humo zimetangaza kuwa, basi moja liligongana na lori lililobeba mazao ya kilimo na kwamba chanzo cha ajali hiyo mbaya ni mvua kali na mtelezo wa barabara.

Maelfu ya watu hufariki dunia kila mwaka nchini Mali kutokana na ajali za barabarani.

Uhaba wa taa za trafiki, barabara mbovu zinazopitika kwa tabu na tabia ya baadhi ya madereva kutojali sheria za barabarani, zinatajwa kuwa miongoni mwa sababu kuu za kutokea ajali za barabarani zinazosababisha maafa ya roho za watu nchini Mali.../