Aug 19, 2021 08:00 UTC
  • Rais wa Algeria: Tunatazama upya uhusiano wetu na Morocco

Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria amesema kuwa, nchi hiyo inatazama upya uhusiano wake na nchi ya Morocco. Rais wa Algeria amesema kuwa, nchi hiyo imefikia uamuzi huo baada ya hatua za hivi karibuni za Morocco ambazo ni za chuki na hasama dhidi ya nchi yetu.

Afisa mmoja wa ngazi za juu wa utawala haramu wa Isreal amezungumzia safari ya hivi karibuni ya Yair Lapid, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala huo nchini Morocco na kubainisha kwamba, moja ya malengo ya safari hiyo ni kuanzisha mstari mmoja wa kijeshi wa Morocco na Israel dhidi ya Algeria.
Hivi karibuni Baraza Kuu la Usalama wa Algeria lilitangaza kuwa, makundi mawili ya kigaidi ya al-Malik na Rashad yamekuwa yakiungwa mkono na madola ya kigeni hususan Morocco na utawala ghasibu wa Israel.

Baraza Kuu la Usalama la Algeria sambamba na kuashiria juhudi zake zinazolenga  kung'oa mizizi ya makundi hayo mawili ya kigaidi limesisitiza kuwa, linafikiria upya uhusiano wake na serikali ya Rabat.

morocco

 

Algeria imekuwa ikiongoza kampeni za kupinga hatua ya Umoja wa Afrika ya kuipasisha Israel kuwa mwanachama mwangalizi wa umoja huo. Katika upande mwingine ikumbukwe kuwa, Morocco ni miongoni mwa nchi za Kiarabu zilizofuata mkumbo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Tags