Aug 26, 2021 03:45 UTC
  • Idadi ya magaidi wa al Shabab waliouawa na jeshi la Somalia yafika 90

Jeshi la Somalia limeripoti kuwa, idadi ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab waliouawa katika oparesheni ya jeshi hilo imeongezeka.

Taarifa ya Jeshi la Somalia imesema, idadi ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab waliouliwa katika shambulio la anga la jeshi la nchi hiyo dhidi ya maficho ya kundi hilo katika eneo la Galmudug katikati mwa Somalia, wamefika 90 na wengine kadhaa wamejeruhiwa. 

Awali jeshi la Somalia lilitangaza kuwa, limeuwa wanamgambo 60 wa al Shabab katika oparesheni iliyofanyika dhidi ya maficho ya kundi hilo huko Galmudug. 

Hili ni shambulio la nne kufanywa na jeshi la Somalia dhidi ya magaidi wa al Shabab tangu kuanza oparesheni za jeshi hilo huko Galmudug.  

Jeshi la Somalia 

Kwa miaka kadhaa sasa Somalia inaendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la al Shabab lilioasisiwa mwanzoni mwaka mwaka 2004. Magaidi wa al Shabab wana mfungamano na kundi la kigaidi la al Qaida na hadi kufikia sasa wameuwa na kujeruhi maelfu ya watu katika mashambulizi mengi yaliyotekelezwa na kundi hilo ndani na nje ya Somalia. 

Tags