Aug 31, 2021 03:42 UTC
  • Tahadhari kuhusu hujuma za kimtandao za utawala wa Kizayuni dhidi ya Algeria

Taasisi ya Utafiti ya Magharibi mwa Asia na Kaskazini mwa Afrika ya Uadilifu na Usawa imetoa taarifa ikitahadharisha kuhusu hujuma kubwa za kimtandao za utawala wa Kizayuni dhidi ya Algeria.

Taasisi ya Utafiti ya Uadilifu na Usawa ya Magharibi mwa Asia na Kaskazini mwa Afrika imesema katika taarifa yake kuwa, utawala wa Kizayuni unapanga kuanzisha hujuma kubwa za kimtandao dhidi ya Algeria. Utawala wa Kizayuni umekusudia kuangamiza miundo msingi muhimu ya serikali ya Algeria kupitia hujuma zake hizo kubwa za kimtandao. Kuvuruga uzalishaji umeme nchini, kushambulia televisheni ya Algeria na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo ni kati ya malengo ya hujuma hiyo ya kimtandao ya utawala wa Kizayuni.  

Taasisi hiyo ya utafiti imesisitiza kuwa, kuna uwezekano benki na masoko ya hisa ya nchi hiyo yakakumbwa na hujuma hiyo ya kimtandao ya Israel dhidi ya Algeria. Imeilitaka pia jeshi la Algeria kuanzisha idara ya kukabiliana na hujuma za kimtandao ili kuzuia kutekelezwa hujuma za  utawala wa Kizayuni.  

Yair Lapid Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni ambaye alifanya safari Morocco kwa lengo la kufungua ofisi ya uwakilishi ya Tel Aviv nchini humo pambizoni mwa ziara yake hiyo alieleza katika kikao na waandishi wa habari kwamba ana wasiwasi na nafasi ya kieneo ya Algeria na hatua ya nchi hiyo ya kupinga Tel Aviv kuwa mwanachama wa Umoja wa Afrika. Matamshi hayo ya Lapid yamekabiliwa na radiamali kali ya viongozi wa Algeria. Viongozi wa Algiers wameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni umeanzisha harakati ya kijeshi dhidi ya Algeria kwa kusaidiwa na Morocco.  

Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni 

Morocco na utawala wa Kizayuni mwaka jana zilitangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida kati yao kufuatia jitihada za rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. 

Tags