Sep 03, 2021 11:44 UTC
  • Nigeria yafunga shule zote katika majimbo mawili kufuatia kuongezeka utekaji nyara

Serikali nne za majimbo kaskazini na katikati mwa Nigeria zimetangaza vizuizi na hatua kadhaa kwa wakazi wa majimbo hayo katika jitihada za kukomesha vitendo vya utekaji nyara na jinai nyingine za utumiaji nguvu zinazoyaathiri maeneo hayo.

Magenge ya wahalifu ya majambazi katika maeneo hayo yamekuwa yakiuwa raia kwa miaka kadhaa sasa; hata hivyo vikosi vya usalama hivi karibuni vimejaribu kukabiliana na uhalifu huo katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa Nigeria. 

Gulio la kuuzia ng'ombe kwa wiki mara moja limesitishwa tangu Jumatano iliyopita katika jimbo la Niger. Hayo yameelezwa na Ahmed Matane msemaji wa serikali ya mtaa. Ameongeza kuwa, uuzaji wa mafuta ya petroli umesitishwa sambamba na kuzuiwa kutumiwa madumu ya chuma katika vituo vya kuuzia mafuta katika baadhi ya maeneo. 

Matane amesema sasa ni marufuku kubeba watu watatu katika pikipiki moja na kusafirisha ng'ombe kwa kutumia lori kuelekea katika maeneo mengine ya nchi. 

Maafisa usalama wa Nigeria wamesema kuwa, wanatambua usumbufu uliojitokeza na kwamba hatua kama hizo zilihitajika ili kuwanusuru watu na mauaji na maaafa yanayosababishwa na  majambazi. 

Wahalifu wenye silaha huko Nigeria 

Katika siku za karibuni pia hatua sawa na hizi zilichukuliwa katika majimbo ya Katsina, Kaduna na Zamfara huko Nigeria. Baadhi ya wahalifu wamekuwa wakiwateka nyara watu kwa umati wengi wakiwa wanafunzi wa shule za sekondari na upili huku wakilazimisha wazazi kuwapa mlungura ili wawaachie huru mateka. 

Tags