Sep 09, 2021 12:41 UTC
  • Maelfu ya Wakenya wataka kuelekea Saudia kutafuta kibarua licha ya manyanyaso wanayokumbana nayo

Licha ya simulizi za kuatua moyo kuhusu madhila wanayopitia wakiwa huko Saudi Arabia, maelfu ya Wakenya wamekwama Nairobi wakilalamikia kuchelewa kupata tiketi ya ndege kwenda kufanyia kazi Uarabuni.

Muungano wa Kupigania Maslahi ya Wafanyakazi Wahamiaji Nchini Kenya (ASMAK) unakadiria kuwa idadi hiyo ni karibu watu 10,000 ambao walifuzu kutoka Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Kozi Fupi (NITA), Nairobi.

Mafunzo hayo yaliyoanzishwa mwakka 2018 hutolewa kwa wahamiaji ambao wamepata kazi Uarabuni na wako tayari kuondoka kuelekea huko.

Ingawa vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti ukatili ambao wafanyakazi wa kigeni hususan kutoka Afrika na mashariki mwa Asia hutendewa katika nchi za Uarabuni hasa Saudia, Oman na Umoja wa Falme za Kiarabu mawakala wa wafanyakazi wanaosaka ajira katika nchi hizo wamelalamika kuwa hakuna ndege za kuwawezesha kuelekea Uarabuni kwa muda wa mwezi mmoja uliopita.

Wakenya wengi wamekuwa wakielekea Uarabuni kufanya kazi za majumbani, ujenzi na kadhaliika. Mara nyingi wanawake huajiriwa kwa mikataba ya miaka miwili kama wafanyakazi za ndani huku wanaume wakihudumu kama wafanyakazi kwenye mahoteli, vibarua, kazi za ujenzi na wanaowaelekeza wateja au kusafisha maduka makubwa. Wanawake wengi hujikuta wakinyimwa mishahara yao na kunyanyaswa kingono.

Wanawake wange wanaokwenda kufanyakazi Saudia hunyanyaswa kingono..

Baadhi yao pia wameishia kuuawa na kuzamisha jamaa zao kwenye lindi la ukiwa huku wengine wakiteswa na kuokolewa, wakirejea nchini mikono mitupu licha ya kuwa na matumaini ya kupata utajiri.

Aidha Wakenya wengine ambao wamefanya kazi na kumaliza kandarasi zao nao pia wamekwama Saudia na hawawezi kurejea nchini kutokana na ukosefu wa ndege. Hii ni kwa sababu ndege ambazo zilikuwa zikiwapeleka Saudia hazikuendeleza safari hizo tangu Agosti.

Tags