Sep 15, 2021 02:35 UTC
  • Zaidi ya wafungwa 100 walitoroka jela Nigeria, watiwa mbaroni

Afisa mmoja wa idara ya jela ya Nigeria ametangaza habari ya kukamatwa zaidi ya wagunwa 100 waliototoka jela nchini humo.

Afisa huyo wa idara ya jela ya Nigeria alitangaza habari hiyo jana Jumanne na kuongeza kuwa, askari wa kulinda usalama wa nchi hiyo wamefanikiwa kuwatia mbaroni wafungwa wasiopungua 108 kati ya 240 waliokuwa wametoroka jela.

Jumapili usiku, afisa huyo wa idara ya jela za Nigeria alisema kuwa, kundi moja la watu wenye silaha lilishambulia jela ya Kaba katika jimbo la Kogi katikati ya nchi hiyo na kuwatorosha wafungwa 240. Alisema mwanajeshi mmoja na askari magereza mmoja waliuawa kwenye shambulizi hilo.

Moja ya jela za Nigeria

 

Kabla ya hapo pia maafisa katika jimbo la Nigeria la Kogi  walisema kuwa, wafungwa 240 wametoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia gereza katika eneo la Kabba-Bunu. Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria imesema katika taarifa yake baada ya tukio hilo kwamba,  washambuliaji walikuwa wamejihami kwa silaha.

Taarifa zilisema kuwa, wakati wavamizi walipofika, walikabiliana na walinzi wa gereza, na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani ya gereza baada ya kuwazidi nguvu askari wa gereza hilo.

Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria imesema kuwa, kulikuwa na jumla ya wafungwa 294 katika gereza hilo wakati shambulio lilipotokea, na kwamba, 240 kati yao walikuwa wakisubiri kesi zao, na 70 walikuwa tayari wameshahukumiwa.

Tags