Sep 16, 2021 08:00 UTC
  • Baraza la Usalama lapasisha azimio kuhusu bwawa la Reinassance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio na kuzitaka Misri, Ethiopia na Sudan kuanzisha mazungumzo kuhusu bwawa la Reinassance.

Azimio lililopasishwa na Baraza la Usalama linaeleza kuwa: Misri, Ethiopia na Sudan zinapasa kuanzisha mazungumzo ili kufikia muafaka utakaoridhiwa na pande zote kuhusu bwala la Reinassance na namna ya kulijaza maji.  

Wakati huo huo ikijibu hatua ya Baraza la Usalama la UN ya kupasisha azimio kuhusu bwala la Reinassance, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imetangaza kuwa: Sisi hatutambui madai yatakayotolewa kwa mujibu wa azimio hilo kuhusu bwawa la Reinassance.  

Mariam Sadiq al Mahdi Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan pia ametoa radiamali yake kufutia azimio hilo lililopasishwa na Baraza la Usalama kwa kusema: Khartoum kwa mara nyingine tena inatangaza kuunga mkono juhudi za usuluhishi za Umoja wa Afrika ili kusaidia kufikiwa muafaka kuhusu bwawa hilo. Amesema Sudan inataraji kuwa mazungumzo kuhusu bwawa la Reinassance yataanza wakati wowote kuanzia sasa chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika. 

Mariam Sadiq al Mahdi 

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa; azimio lililopasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaiagiza Ethiopia kushiriki kwa dhati katika mazungumzo ili kufikia muafaka kuhusu bwawa hilo tajwa.