Sep 16, 2021 08:05 UTC
  • Ufaransa yadai kumuua kiongozi wa Daesh katika eneo la Sahel

Rais wa Ufaransa ametangaza habari ya kuuliwa kiongozi wa magaidi wa kundi la Daesh katika eneo la Sahel.

Rais Emmanuel Macron amedai kuwa wanajeshi wa Ufaransa wamemuua Adnan Abu Walid al Sahrawi kiongozi wa magaidi wa kundi la ukufurishaji la Daesh katika eneo la Sahel barani Afrika. Rais wa Ufaransa amekutaja kuuliwa Adnan al Sahrawi kuwa mafanikio makubwa katika kupambana na kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la Sahel barani Afrika. 

Al Sahrawi alikuwa kiongozi wa moja ya matawi ya kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la mpaka na Mali, Burkina Faso na Niger ambayo yamefanya hujuma nyingi za kigaidi. Al Sahrawi mwaka 2015 alitangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh; na kundi lake lilikuwa likihesabiwa kuwa moja ya matawi ya kigaidi ya Daesh athirifu zaidi  barani Afrika; ambalo mwaka 2019 na 2020 lilifanya mashambulizi mengi. 

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni walisisitiza kuwa, Afrika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2021 imedhurika na kujipenyeza pakubwa makundi ya kigaidi ya Daesh na al Qaida.

Magaidi wa al Qaida 

Wamesema, kujipenyeza pakubwa makundi ya kigaidi ya Daesh na al Qaida katika baadhi ya nchi za Kiafrika kama Mali, Burkina Faso, Kodivaa, Niger, Senegal, Nigeria, Cameroon, Somalia, Kenya, Msumbiji na Tanzania ni jambo lenye kutia wasiwasi. 

Tags