Sep 16, 2021 13:35 UTC
  • Hassan Wario
    Hassan Wario

Habari za karibuni zinasema kuwa, aliyekuwa Waziri wa Michezo wa Kenya Hassan Wario sasa yuko huru baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 3 saa chache baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kuhusiana na sakata ya Rio 2016.

Hassan Wario na afisa zamani wa Kamati ya Olimpiki ya Kitaifa ya Kenya (Nock) Stephen Soi, walikuwa wamepatikana na hatia ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka kuhusiana na kashfa ya Olimpiki ya Rio 2016. 

Wario amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya shilimgi milioni 3.6 kwa kuhusika kwake katika kashfa hiyo.

KKwa upande wake, afisa zamani wa Kamati ya Olimpiki ya Kitaifa ya Kenya (Nock) Stephen Soi anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 103 za Kenya kwa madai ya matumizi mabaya ya pesa za umma.

Wawili hao walikuwa katika mahakama ya Milimani mapema leo Alhamisi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Kupambana na Ufisadi, Elizabeth Juma ambapo walisomewa hukumu hiyo.

Hassan Wario

Miongoni mwa mashtaka wanayokabiliwa nayo ni pamoja ubadhirifu wa malipo ya marupurupu, ununuzi wa tiketi za ndege kwa watu wasioidhinishwa, na kutumia vibaya fedha zilizokutengwa kwa ajili ya timu ya Olimpiki huko Rio. Wario alihudumu katika Baraza la Mawaziri la kwanza la Rais Uhuru Kenyatta hadi 2018 alipoteuliwa kuwa balozi wa Kenya nchini Austria.

Alirejea nchini Kenya kimya kimya wakati kesi yake ilipokuwa ikiendelea. Uhuru baadaye alimtimua afisini na nafasi yake ikachukuliwa na balozi Robinson Githae mnamo Mei 2019.

Tags