Oct 13, 2021 02:30 UTC
  • Kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa Tunisia

Hatimaye baada ya vuta nikuvute ya kisiasa ya majuma kadhaa nchini Tunisia, serikali mpya ya nchi hiyo imeapishwa ikiongozwa na mwanamama Najla Bouden Romdhane.

Bi Najla anakuwa mwanamke wa kwanza, kushika nafasi ya Waziri Mkuu nchini Tunisia. Dakta Bouden, mwenye umri wa miaka 63 kama alivyo Rais Saied, anakuwa waziri mkuu wa 11 wa Tunisia tangu mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyohitimisha utawala wa kidikteta wa  Zine El Abedine Ben Ali na kuchochea kile kilichojulikana kama Machipuo ya Kiarabu.

Akizungumza katika hafla ya kula kiapo, Waziri Mkuu mpya wa Tunisia ametangaza kuwa, kipaumbele cha baraza lake la mawaziri ni kurejesha imani ya wananchi kwa serikali na kkufanya juhudi za kuhuisha imani ya jamii ya kimataifa kwa serikali ya Tunisia. Filihali yamepita mamuma kadhaa tangu mgogoro wa kisiasa nchini Tunisia ulipoibuuka. Takribani miezi miwili iliyopita, Rais Kais Saied alimuuzulu Waziri Mkuu, akalisimamisha bunge na kuhodhi madaraka yote ya utendaji. Si hayyo tu, bali Rais wa Tunisia aliwafuta kazi baadhi ya mawaziri katika serikali yake na kuondoa kinga ya kisiasa kwa Wabunge.

Hatua na maamuzi hayo ya rais Kais Saied yalikabiliwa na malalamiko makuubwa ya baadhi ya vyama vya siasa vyay Tunisia ambavyo vilitaja maamuzi hayo kuwa ni mapinduzi dhidi ya katiba. Katika kutetea maamuzi na hatua zake hizo, Rais wa Tunisia alidai kwamba, amefanya hivyo kutokana na kuongezeka ufisadi, usimamizi mbaya katika kukabiliana na janga la Corona na kushtadi hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo.

Rais Kais Saied na Waziri Mkuu Najla Bouden Romdhane

 

Pamoja na haya,hatua za Rais Kais Saied hususan kurefuka muda wa kufungwa kazi za Bunge na kuchaguliwa Waziri Mkuu mpya, kuliifanya anga ya Tunisia iendelee kushuhudia mwenendo wa kuuongezeka maandamano na malalamiko ya wananchi. Wasiwasi mkubwa wa wananchi wa Tunisia ni kuharibika matunda ya vuguvugu la wananchi la mwaka 2011 na kuingia dosari mchakato wa demokrasia kuchukuua mkondo wake katika nchi hiyo. Ni kwa kuzingatia ukweli huo, ndio maana waliendelea kujitokeza mabarabarni kwa majuma kadhaa kupinga na kulalamikia maamuzi ya Rais huyo.

Mkusanyiko na maandamano ya karibuni kabisa ya wananchi wa Tunisia ni yake ya siku tatu zilizopita, ambapo maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika mji mkuu Tunis.  Seikali mpya ya Tunisia ikiongozwa na Waziri Mkuu Najla Bouden Romdhane imeanza kazi baada ya mgogoro mkubwa. Kuchaguuliwa waziri Mkuu mwanamke kumekabiliwa na radiamali mbambali. Neji Jalloul, waziri wa zamani wa Tunisia na Mkuu wa Muungano wa taifa wa Tunisia sanjari na kuashiria kwamba, kuteuliwa mwanamke kwa ajili ya kushika wadhifa wa Waziri Mkuu ni chaguo zuri amesema,  mafanikio yakke katika hatua ya sasa iliyoko mbele yake yatakuwa ni mafanikio ya nchi na taifa la Tunisia.

Rais Kais Saied wa Tunisia 

 

Bi Najla Bouden Romdhane ameanza kuhudumu kama Waziri Mkuu katika hali ambayo, hali mbaya ya uchumi, ufisadi, kueneza maradhi ya Covid-19, uhaba wa dawa katika sekta ya tiba na afya na mizozo ya kisiasa, imeshadidisha mpasuko wa kisiasa na kuifanya nchi hiyo kukabiliwa na wingu zito la mgogoro. Katikka fremu hiyo, Waziri Mkuu wa Tunisia ameliambia baraza lakke la mawaziri kwamba, lina jukumu la kuponya vidonda vya nchi hiyo na kuikoa kuutokkana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi , kifedha na kijamii.

Dkt. Reza al-Shakandali, mtaalamu wa masuala ya kiuchumi sambamba na kuaashiria kwamba, mipango ya serikali mpya itatekelezwa kupitia ramani ya njia iliyobainishwa na Rais Kais na kusema kwamba: Serikali mpya ina kibarua kigumu cha kuinasua nchui hiyo na hali ya sasa ya uchumi uuliovurugika, hata hivyo kufanikiwa katika njia hiyo siyo jambo ambalo haliwezekani.

Alaa kulli haal, Bi Najla Bouden Romdhane amechukua Uwaziri Mkuu akiwa amerithi migogoro na changamoto nyingi ambazo ili kukabiliana nazo panahitajika azma na irada madhubuti ya wanasiasa na wananchi kuuwa pamoja nayye. Mbali na hayo, uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, ni jambo ambalo linaweza kuzidi kuzorotesha na kuifanya kuwa mbaya  hali ya mambo ya nchi hiyo.

Tags