Oct 14, 2021 02:22 UTC
  • Mohamed Abdullahi Mohamed
    Mohamed Abdullahi Mohamed

Rais wa Somalia amesema katika hotuba yake aliyotoa jana Jumatano kwamba, uamuzi uliotolewa siku ya Jumanne na Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusu mzozo wa mpaka na Kenya ni fursa kwa nchi mbili hizo kushirikiana.

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia maarufu kwa jina la "Farmajo"  amebainisha hayo baada ya mahakama ya ICJ kutoa uamuzi kwa maslahi ya Somalia kwa kuipatia nchi hiyo mamlaka ya kusimamia eneo la kistatretejia tajiri kwa mafuta na gesi katika bahari ya Hindi.  

Rais wa Somalia amesema Kenya inapasa kuuchukulia uamuzi wa mahakama ya ICJ kama fursa ya kuboresha uhusiano kati ya nchi mbili na kushirikiana watu wa nchi hizo jirani. Amesema Somalia haikuchagua kuwa jirani ya Kenya bali ni matakwa ya Mwenyezi Mungu na tunalazima kuishi kwa amani kama majirani wema. 

Huko Mogadishu wananchi wa Somalia wameupokea kwa mikono miwili uamuzi wa mahakama ya ICJ baada ya kesi hiyo kuendeshwa kwa muda wa miaka saba.

Kenya iliithumu Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuwa inaegemea upande mmoja na kupinga mamlaka ya kisheria ya mahakama hiyo ya kutoa maamuzi na hukumu kabla ya  kutoa uamuzi wake Jumanne wiki hii na kuipatia Somalia mamlaka ya kusimamia eneo hilo la kistratejia katika ukanda wa bahari ya Hindi.

Jana Jumatano  Rais Kenyatta wa Kenya alipiga uamuzi huo wa ICJ na kusema  ingawaje Kenya haijashangazwa na uamuzi huo lakini inatiwa wasiwasi na matokeo hasi yatakayosababishwa na uamuzi huo kwa eneo zima la Pembe ya Afrika.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya 

 

Tags