Oct 14, 2021 02:53 UTC
  • Algeria yazima njama ya utawala haramu wa Israel

Vyombo rasmi vimetangaza kuwa, askari usalama wa Algeria wamefanikiwa kuzima njama iliyokuwa imepangwa kutekelezwa na maadui wa nchi hiyo kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Televisheni rasmi ya Algeria imeripoti kuwa, njama hiyo ilianza kupangwa mwaka 2014 na kwamba wiki hii jeshi la Algeria limefanikiwa kuwakamata wahusika kadhaa wa njama hiyo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, lengo la njama hiyo lilikuwa kuteteresha usalama wa Algeria na kwamba ilipangwa kuwa, kundi moja linalotaka kujitenga baadhi ya maeneo la nchi hiyo lingetekeleza njama hiyo likisaidiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi moja ya kaskazini mwa Afrika.

Televisheni ya Algeria imetangaza kuwa ripoti kamili kuhusu njama hiyo itatolewa baadaye ikiambana na ushahidi. 

Itakumbukuwa kuwa tarehe mwezi Agosti mwaka huu Algeria ilikata uhusiano wake na Morocco ikiituhumu nchi iyo na mashirika wake, Israel kuwa zilihusika na moto ulioteketeza misitu ya nchi hiyo na kuua makumi ya raia.  

Tags